News Detail

Featured 22 Aug JE, WAJUA KWAMBA CHUMVI INATUMIKA KATIKA UREMBO?

JE, WAJUA KWAMBA CHUMVI INATUMIKA KATIKA UREMBO?

Chumvi

 

PAMOJA na kutumiwa kama kiungo katika mapishi mbalimbali, chumvi ina umuhimu wake katika urembo.

Chumvi inaweza kutumika kama kipodozi na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia.

Kumekuwepo na sababu mbalimbali zinazosababisha warembo kupata matatizo ya ngozi.

Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta ya kupindukia usoni na hata mlundikano wa ngozi zilizokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kuwapa hamasa ya hata kutumia vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.Huwa ni vipodozi vyenye kemikali hatari.

 

Kwa kutambua hilo, wataalamu wa urembo wa kiasili walikuja na njia hii ambayo haina gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo wengi.

Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika kutatua matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanalolifahamu hili.

Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.

 

Mahitaji / Vinavyohitajika:

Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwa

 

Namna ya kufanya

  • Nawa uso wako kwa maji ya kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi. Chovya kwenye chumvi na kisha sugua katika uso taratibu.

  • Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue kwa kutumia mikono yako. Fanya hivyo hadi utakapoona uchafu unatoka. 

  • Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji baridi.

 

Unashauriwa kufanya aina hii ya ‘scrub’ mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.

Hata hivyo, utumiaji wa chumvi usoni kwa muda mrefu unaweza kukausha ngozi sana.

Hivyo inafaa kutumika mara moja kwa wiki kisha baadaye unapaka 'moisturizer' kwa wingi.

>>>>