News Detail

22 Aug JE ,UNAFAHAMU UMUHIMU NA  FAIDA ZA KUNYWA MAJI KWA WINGI?

JE ,UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA ZA KUNYWA MAJI KWA WINGI?

Ni asubuhi njema nyingine mwenyezi Mungu kaniamsha salama?
Pembeni nina glasi yangu ya maji safi ya kunywa!


Kabla sijapiga mswaki napendelea kunywa glasi moja ya maji....Ni muhimu sana!!
Kuna watu wanajiita warembo lakini hawajui umuhimu wa maji na hawapendi kunywa maji kabisa! Wakienda sehemu kitu cha kwanza kuagiza ni soda au juice?
Maji kwao wanayaona kama dawa wanakunywa pale tu wanapojisikia kiu ya maji! Mnakosea!!❌
Maji ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na yana faida zaidi kwa wana urembo.
Leo naomba nikupe faida chache tu za maji katika miili yetu na urembo wetu?
Nimeandika faida4 na jinsi ya kunywa maji kulingana na faida unayopata!
Soma kwa utaratibu na uelewe ni muhimu sana!

FAIDA ZA MAJI
1. Maji yanasafisha ngozi
-kunywa glasi moja asubuhi kabla ya 
ya kupigwa mswaki
-kunywa glasi mbili baada ya chai
-mchana kunywa glasi mbili 
-Jioni glasi mbili
-usiku baada ya chakula kunywa glasi moja
-Na kabla ya kulala kunywa glasi mbili
-Lala na maji kwenye jagi na ikitokea ukaamka katikati ya usingizi basi kunywa glasi moja
Fanya hivyo kila siku utaona ngozi yako itakavyonawili na kuwa na mwonekano wa afya na hata magonjwa ya ngozi yatapotea yenyewe!


2.Maji huondoa uchafu na sumu mwilini!
Kunywa maji ya kutosha angalau lita2 na nusu kwa siku!
-asubuhi nusu lita
-mchana lita moja
-jioni nusu lita
-usiku nusu lita
Utakua unakojoa mara kwa mara hiyo ni figo inasafishika na mkojo wako utakua mweupe ni dalili kua uchafu umesafishwa na hata jasho lako halitakua na harufu kali, harufu mbaya ya kinywa itaisha pia


3. Maji hupunguza mwili na tumbo
Kunywa maji angalau lita3 kwa siku!
-asubuhi kabla ya kula chochote kunywa maji nusu lita yenye umoto unaweza ukakamulia na ndimu ama asali au vyote!
-mchana kunywa maji nusu lita nusu saa kabla ya kula 
-na kunywa lita moja nusu saa baada ya kula
-jioni kunywa maji nusu lita nusu saa kabla ya kula
-na usiku baada ya kula kunywa nusu lita ya maji yenye umoto 
Utapungua taratibu but kwa uhakika...tumbo na mwili kwa ujumla! Na magonjwa yasiyo rasmi yataisha 


4.Maji hurekebisa joto la mwili 
-kunywa maji angalau lita2 kwa siku

↗️Kila cell/chembe hai ya mwili wako inahitaji maji!
Kwahiyo jiweke utaratibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku!
MAJI NI UHAI?
MAJI NI UREMBO?
MAJI NI AFYA?
⭕️Hakikisha unakunywa maji safi na salama

Like n share?

>>>>