News Detail

Featured 22 Aug Je unasumbuliwa na WEUSI wa KWAPANI na JASHO lenye harufu kali ?

Je unasumbuliwa na WEUSI wa KWAPANI na JASHO lenye harufu kali ?

Huenda umetumia deodorant na manukato mbalimbali ili kudhibiti tatizo hilo lakini hali imezidi kuwa mbaya na imeshindikana kumaliza tatizo! 
Ondoa shaka! ?tupo  t  tupo hapa kukusaidia


Hapa nitakuelekeza jinsi ya kutengeneza mchanganyiko utakao ondoa kabisa tatizo hilo!


?Usafi ni muhimu sana kama njia moja wapo ya kudhibiti tatizo
??Hakikisha unapata mda mzuri wa kuoga vizuri kwa utaratibu angalau mara2 kwa siku na kila unapooga hakikisha unajisafisha makwapani kwa sabuni, dodoki laini la kuogea na kujisuuza kwa maji ya kutosha! 


?Kabla ya kuanza kutumia mchanganyiko huu achana na deodorant za madukani na tiba zote ulizotumia awali...
✂️Usisahau kunyoa nywele zote za kwapani na oga kwa kusafisha kwapa kama nilivyokuelekeza mwanzo kila unapotaka kutumia mchanganyiko huu.
Sasa naenda kueleza hatua jinsi ya kutengeneza na namna ya kutumia mchanganyiko

No photo description available.
MAHITAJI 


1. Baking soda kijiko1 na nusu 
2. Limao/ndimu 
3. Bakuli dogo la kuchanganyia 

 

JINSI YA KUTENGENEZA 


Kata limao/ndimu katikati...chukua bakuli uweke baking soda kijiko1 afu ukamulie kipande kimoja cha limao/ndimu afu malizia nusu kijiko cha baking soda kisha changanya kwa kijiko hadi ichanganyike vizuri. Hapo mchanganyiko wako utakua tayari kutumia 
?Mchanganyiko hautakiwi kukaa mda mrefu kwahiyo hakikisha unatumia mara tu baada ya kuuchanganya!?

 


JINSI YA KUTUMIA 


Chota mchanganyiko kidogo kidogo kwa mkono na ujisugulie kwapani kila moja kwa mda wa dakika 3. Baada ya hapo oga au jioshe makwapa kwa maji mengi!


Fanya hivyo kila siku utaanza kuona matokeo mazuri na kwa mda usiozidi wiki mbili tatizo litakua limekwisha kabisa!

Like n share?

 

>>>>